Mwenyekiti wa baraza la Elimu ya watu wa Wazima Dr. Naomi Katunzi amewataka wasomi Nchini kutumia elimu waliyoipata kusadia na kutatua changamoto mbalimbali zilizopo katika jamii
Dr. Naomi ameyasema hayo wakati wa mahafali ya 61 ya Elimu ya watu wazima yaliyofanyika Kampasi ya Morogoro ,ambapo amesema kuna haja ya wasomi kuwa mfano katika jamii kwa kutumia ujuzi walionao ili kusaidia jamii
Anasema serikali na wananchi kwa ujumla wanawategemea wasomi katika masuala mbalimbali ikiwemo utafiti,ujuzi na elimu ya maisha hivyo ni jukumu lao kuonesha utofauti kati yao na makundi mengine.
Ameongeza kuwa kitendo cha serikali kuruhusu wanafunzi waliopata ujauzito kuendelea na masomo kumeongeza morali kwa taasisi hiyo kuendelea kutoa elimu kwa watu wazima .
Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi waliohitimu katika chuo hicho wameipongeza serikali katika masuala ya elimu hasa kuwajali kutoa fedha za ujenzi wa madarasa, maabara na ajira za walimu .
Naye Mkuu wa Taasisi ya elimu ya watu wazima Profesa Maiko Ng’umbo amesema mpango wa taasisi hiyo kuongezà Kampasi zingine mbili mikoa ya Arusha na Tanga ili kuongeza wigo kwa wtu kujiendeleza kielimu kwani kwa sasa kuna kampasi tatu tu ambazo ni Morogoro,Mwanza na Dare salaam.
Anasema Muamko wa elimu kwa wanawake umeongezeka kwani zaidi ya asilimi 70 ya wahitimu mwaka huu ni wanawake jambo ambalo linatia moyo kwa taasisi kuwafikia watu wengi zaidi ili watimize ndoto zao.
Katika mahafali hayo Jumla ya wanafunzi 1566 wamehitimu fani mbalimbali na kutunukiwa vyeti ambapo mahafali hayo yamejumuishwa wanafunzi kutoka kampasi ya Daresalam,Mwanza na Morogoro.