Habari za Mastaa

Wastara na miaka saba ya kifo cha Sajuki, akumbuka haya

on

Siku kama ya leo miaka saba iliyopita tasinia ya filamu ilimpoteza moja ya mtu aliyepata umaarufu kupitia kazi ya sanaa ya maigizo, Juma Issa Kilowoko maarufu kama Sajuki aliyefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu, ikiwa leo ni kumbukumbu ya kifo chake mke wake Wastara amekumbuka moja ya jambo alilowahi kushare na marehemu kabla ya umauti haujamkuta.

Wastara ameshare ilivyokuwa siku moja kabla umauti haujamkuta Sajuki kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameandika…”“Nakumbuka siku ya tal 1/1/2013 Sajuki alikuwa amelazwa muhimbili hosptal Aliniambia unajua mke leo nimeuona mwaka mpya hata nikifa mda huu nitasema na mimi nilikufa mwaka mpya afu akasema mke wangu unajua imebadilika number tu lakini maisha ni yaleyale kilakitu kiko vilevile na mimi niko hapa hapa ktandani sina hata mabadiliko walau ningeweza kuinuka tu nikakupeleka out ningesema mwaka umekuwa mpya na mambo mapya”

“Hii kitu imeniharibu sana sionagi kwangu kama mwaka mpya ni kitu kipya ila naona ni kitu chenye kumbukumbu mbaya sana kwangu watu wanaumiaga kufiwa na wazazi na mume lakini mimi kwangu huyu jamaa alikuwa mguu wangu wa pili uliokatika nikaona yeye ndio amesimama kwenye hiyo nafasi nilijiona mzima na nina miguu yangu yote 2 na sijawahi kujiona kuwa nina mapungufu ya mguu mmoja mpka siku alipoondoka mume wangu kipenzi sajuki ndio niliona mapungufu yangu yooote hata mengine nilijiongezea tu mwenyewe akilini mwangu”

“Watoto wako wanakuombea sana mimi sijaaacha kukuombea na sitaacha mpka siku nitakayo kuja huko ulipo ulimuacha bint yako mdogo wa miezi 7 sasahivi amekuwa na anajua ulikuwepo na umeondoka anakuombea kilasiku ili urudi ajui kama wewe auwezi kurudi ila sisi ndio tutakuja ulipo Tunakupenda sajuki wetu mungu akulaze mahali pema peponi amiin amiin sote tuseme amiin tuendelee kumuombea”

Soma na hizi

Tupia Comments