Mix

Wataalam watoa mawazo kuhusu uboreshwaji wa soko la Kariakoo

on

Jumamosi ya July 10 2021 ni moja kati ya siku ngumu kwa wafanyabiashara wa soko la Kariakoo ambapo siku hiyo sehemu kubwa ya soko la Kariakoo liliteketea kwa moto.

Mawazo mbalimbali yamekuwa yakitolewa kuhusiana na soko hilo namna ambavyo ukarabati unaweza kufanyika.

Jengo hilo la soko la Kariakoo lililojengwa 1974 wengi wanataja kuwa lina historia kubwa Tanzania hususani katika jiji la Dar es Salaam, wadau wa tasnia ya majengo wametoa mawazo tofauti tofauti kuhusiana na hilo.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa kituo cha urithi na usanifu wa majengo Dar es Salaam (DARCH) Aida Mulokozi amenukuliwa akisema.

“Jengo la soko lilikamilika 1974 na lina umbo lenye mfano wa kijiji chini ya mti, paa lake lenye miamvuli ya kipekee linaleta kimvuli cha kufurahisha”

Jengo la soko la Kariakoo lilibuniwa na msanifu majengo Beda Amuli ambaye alikuwa mwafrika wa kwanza kusajiliwa kama msanifu majengo na kuanzisha kampuni ya usanifu baada ya Uhuru.

Mbunifu majengo na Rais wa Chama cha Wabunifu Majengo Tanzania (AAT) David Kibebe ametoa mawazo yake kuhusu soko hilo la Kariakoo baada ya kuungua.

Hii ni picha ya soko la Kariakoo ilipigwa 2012 na Bene Redmann

Kariakoo Market Hall, Dar es Salaam, Tansania
Archiktekt: Beda j.Amuli
Fertigstellung 1974

“Ni wajibu wetu kama wataalam kuhakikisha kwa kila linalowezekana linafanyika kutathmini uharibifu wa jengo ulitokana na moto huu ili kulirejesha kama lilivyokuwa awali”

Rais wa chama cha waandisi Tanzania (ACET) Mhandisi Deo Mugishagwe >>> “Jiji halina miundombinu ya uhakika ya kudhibiti matatizo kama haya kutokea tena kwenye majengo ya kijamii”

AAT, ACET na DARCH kama mashirika na vyama vya kitaaluma wanakaribisha taasisi husika, wamiliki na Uongozi wa soko la Kariakoo kukutana ili kushirikiana kurejesha muonekano wa soko la Kariakoo.

Tupia Comments