Kulingana na Ben Saul, ripota maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uendelezaji wa haki za binadamu na kupambana na ugaidi, ametoa wito kwa Israel kufuta sheria mbili zinazozuia shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi wa Kipalestina “kutekeleza majukumu yake ya kimataifa ya kutoa misaada ya kibinadamu na huduma muhimu”.
Mwezi Oktoba mwaka jana, bunge la Israel lilipitisha miswada miwili iliyolaaniwa vikali, na kupiga marufuku operesheni za UNRWA nchini Israel.
Katika ripoti iliyochapishwa Februari 19, Saul na wataalam wengine 24 huru wa Umoja wa Mataifa walisema “vifungu fulani katika sheria hizi” – ambavyo vilianza kutumika mwishoni mwa mwezi uliopita – vinaweza kukiuka sheria za kimataifa.
Ripoti hiyo pia ilionya kwamba “kusambaratisha UNRWA nje ya mchakato wa kisiasa unaojumuisha kuhitimisha kwa utaratibu wajibu wa Shirika hilo” kunaweza kuhatarisha “kudhoofisha usitishaji mapigano” kati ya Israel na Hamas.