Top Stories

“Watakaopewa mimba ruksa kurudi shule” Ndalichako

on

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema Wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari watakaokatisha masomo yao kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo utoro, mimba na changamoto mbalimbali za kifamilia watapewa fursa ya kurejea Shuleni katika mfumo rasmi.

Waziri Ndalichako ametoa kauli hii leo akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma kuhusu mafanikio ya Sekta ya elimu katika kipindi cha miaka 60 “leo natoa waraka wa elimu ambao utaelezea ni lini Wanafunzi watakaokatisha masomo kwa sababu ya mimba na changamoto nyingine watapaswa kurejea Shuleni, leoleo natoa waraka hakuna kupoa, zege halilali”

Wizara ya Elimu inaelezea mafaniko yake ndani ya miaka 60 ya Uhuru kwa kutumia hashtag ya “Tunaboresha Elimu yetu”

WAVAMIZI WAUA TWIGA, SWALA “WACHOMA SHAMBA, MALI ZAIDI MILIONI 60 ZATEKETEA”

Soma na hizi

Tupia Comments