NI Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa ambae leo Septemba 4, 2021 amekutana na Waandishi wa Habari kuzungumza mambo mbalimbali yakiwemo Chanjo ya Corona iliyotolewa kwa Watanzania.
“Tangu zoezi la chanjo lianze zaidi ya Watanzania 325,000 sawasawa na asilimia 31.5 ya chanjo zilizoletwa wameshapokea chanjo, zoezi linakwenda vizuri Watanzania wanaendelea kujitokeza kupata chanjo na Serikali inaendelea kuhimiza ambao hawajachanja wakachanje lakini msisitizo ni kwamba jambo hili ni hiari”——— asema Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa.