Jamii imehimizwa kushirikiana kuwa karibu na wasaidizi wa kisheria chini ili kuwalinda wasichana na ndoa za utotoni ambazo huchochea umaskini, maradhi na ujinga.
Meneja Programu wa kitu cha Wasaidizi wa Kisheria mkoani Shinyanga, Be John Shija alitoa wito huo baada ya kuingilia Kati mpango wa Lyuba Seif na Familia yake wa kumuoza binti Yake Kati umri mdogo.
“Kutokana na mkakati huu hatua za haraka zilichukuliwa ili kumnusuru binti huyu asiolewe kwa kulazimishwa akiwa katika umri mdogo na kupoteza kabisa mdoto zake za maisha,” alisema.
ndoa za utotoni zimekuwa ni tatizo kubwa ambalo huwazulumu mabinti wadogo haki zao za msingi katika maisha.
Wasaidizi wa kisheria katika kila wilaya wamekuwa wakifanya kazi kubwa sana ya kuwasaidia wale wanadhulumiwa haki Zao za Kisheria na pia kutoa elimu juu ya masuala mbalimbali ya Kisheria katika maeneo hayo.
Taarifa hizi za mpango wa Bw Seif kumuoza binti yakeziliwafikia watoa huduma za msaada wa kisheria na ilikuwa bahati kwani mpango huu haukuwa umefika hatua ya mbali zaidi.
Ili kuzuia mpango huo kuendelea hatua za haraka zilichukuliwa kwa ushirikiano na raia wema katika kijiji hicho.
Kituo cha PACESHI kilichukua hatua muhimu kumuelimisha Bw Seif juu ya masuala ya Kisheria na haki as watoto na hasa kupata elimu.
PACESHI ni shirika la wasaidizi wa kisheria chini ya ufadhili wa Legal Services Facility (LSF), shirika linalotoa ruzuku kwa mashiriika yanayotoa huduma za msaada wa kisheria Tanzania Bara na visiwani Zanzibar chini ya mradi huu Zaidi ya wasaidizi wa kisheria 3700 walioko kila wilaya wameendelea kutoa msaada wa kisheria kwa jamiii.
Kwa wastani kwa mwaka wasaidizi wa kisheria ushughulikia
Kwa upande wake Ms Theresia Masinga, manage ni mwalimu wa chuo cha VETA Shinyanga alisema tangu siku ya kwanza binti huyu alipoanza mafunzo ameonyesha bidii kubwa sana na kuwa jitihada hizi ni kiashiria cha malengo aliyojiwekea katika maisha.
Binti huyu as Mzee Seif anawakilisha sehemu ndogo sana ya mabinti Wengi ambao wamekuwa wakidhulumiwa haki zao za msingi za kupata elimu.