Watu watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wameuwawa na Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma katika barabara ya Heru shingo wilaya Kasulu baada ya Askari polisi wakiwa katika doria ya kubaini,kuzuia na kutanzua uharufu ambapo majambazi hao walikua wanafanya unyang’anyi kwa abiria kwa kufunga barabara.
Akiongelea tukio hilo Kaimu Kamanda wa polisi Mkoani Kigoma ACP Iddy Kiyogomo amesema tukio hipo limetokea February 20,2025 saa 12 Alfajiri eneo la katundu heru shingo majambazi wakitumia siraha aina ya AK 47 kufanya unyang’anyi huo ambapo yalitokea majibizano ya risasi baina ya polisi na majambazi.
Katika tukiko hilo siraha mbili aina ya AK47, magazine 02 na risasi 52,siraha za jadi,panga 02 na marungu yamepatikana katika tukio hilo baada ya majibizano ya kurushiana risasi kupekekea majambazi watatu kuuwawa.
Polisi Kigoma wanasema hadi sasa majambazi hao hawajatanbuliwa majina wala anuani za makazi na wameuwawa baada ya kujeruhiwa kwa risasi, miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali ya Wilaya ya Kasulu kwa utambuzi.
Aidha Jeshi la Polisi Kigoma linaendelea kuwaomba wananchi kufanya Shughuli halali za kujiingizia kipato zinazotambulika kwa mujibu wa sheria.