Ad
Ad

Top Stories

Watatu wauawa kisa ikidaiwa ni dini

on

Polisi Mkoani Kagera wanaendelea kufanya uchunguzi wa tukio la vifo vya Watu watatu wa Familia moja ambalo limetokea katika Kijiji cha Mayondwe Wilayani Muleba Mkoani humo chanzo kikidaiwa kuwa ni imani za Kidini.

RPC wa Kagera Revocatus Malimi amewataja waliopoteza maisha kuwa ni Editha Martin (48), Sawia Sudi (25) na wa tatu ambaye ndiye Mtuhumiwa na Mhusika Mkuu wa vifo vyote Sudi Mwamadi (49) ambaye baada ya kufanya mauji ya Mke wake Editha na Mtoto wake Sawia na yeye alijinyonga juu ya mti kwa kutumia shuka.

RPC Malimi amesema uchunguzi wa awali umebaini kwamba chanzo cha tukio hilo ni ugomvi wa kifamilia uliosababishwa na uamuzi wa Mke na Binti yake ambao mwanzo walikuwa Waislamu lakini wakaamua kubadili dini na kuwa Wakristo jambo lililopingwa na Mtuhumiwa na kusababisha kuwepo kwa ugomvi wa mara kwa mara mpaka kufikia hatua ya kuwaua kwa panga.

KIJANA MIAKA 27 MIKONONI MWA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMPA MIMBA MWANAFUNZI WA DARASA LA NNE

Soma na hizi

Tupia Comments