Mgahawa maarufu wa Sage Regenerative Kitchen & Brewery huko California Nchini Marekani unaouza vyakula vya mboga mboga umetangaza kufungwa baada ya Wateja wake waaminifu ambao ni waumini wa vyakula vya mboga za majani (Vegeterians) kuandamana vikali kupinga uamuzi wa Mgahawa huo wa kutaka kuanza kuuza nyama na bidhaa za maziwa amnapo Mgahawa huo uliokuwa ukihudumu kwa miaka 14 ulifanya mabadiliko hayo kwa lengo la kuvutia Wateja wapya kufuatia changamoto za kifedha.
Hatua hiyo iliwakasirisha Wateja wa mboga mboha (vegans) ambao waliona ni usaliti wa misingi ya Mgahawa huo huku wengi wakitoa maoni yao mtandaoni wakikosoa uamuzi huo pia Shirika la haki za Wanyama Nchini humo PETA pia liliongeza shinikizo likisema Mgahawa huo umesaliti Wanyama na Wateja wake.
Aidha Mmiliki wa Mgahawa huo, Mollie Engelhart amesema walijaribu kuuza Nyama ili kufufua biashara lakini badala yake walikumbana na ukosoaji mkubwa licha ya jitihada za kuuza Nyumba yao ili kuokoa Mgahawa huo pia hazikufanikiwa.
Baada ya tangazo la kufungwa baadhi ya Watu walishangilia hatua hiyo wakisema ni mkosi baada ya usaliti kwa Wanyama na Wateja wa mboga mboga (vegans) huku wengine wakisikitika kwa kupoteza Mgahawa walioupenda.