Watendaji wa ngazi ya Mkoa katika mkoa wa Lindi wamekula Kiapo na kupewa mafunzo ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao.
Watendaji hao wamekula kiapo cha kutokuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa katika zoezi zima la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.
Watendaji hao wamekula kiapo cha kuzingatia maadili katika zoezi hilo kama walivyoapa kwenye maadili ya utumishi wa umma.
Akizungumza mara baada ya kuwaapisha, Hakimu mkazi mkuu mfawidhi mkoa wa Lindi Consolata Singano alisema kila mtendaji anatakiwa kusimamia zoezi hilo kwa uadilifu uliotukuka.
Akitoa hotuba kwa watendaji hao,Makamu Mwenyekiti wa tume huru ya taifa ya uchaguzi, Mheshimiwa Jaji (R) (MST.) Mbarouk Mbarouk, aliwataka watendaji hao kuwafundisha kwa umahiri wasimamizi wa uandikishaji wa wapiga kura.
Jaji Mbarouk alisema kuwa kila mmoja anatakiwa kufanya kazi kwa weledi na kutumia uzoefu wao kufanikisha malengo ya tume.
Alimalizia kwa kusema kuwa Mawakala wa vyama vya siasa wanaruhusiwa kushiriki zoezi la kuandikisha wapiga kura lakini hawataki wa kuingilia majukumu ya watendaji wa tume ya uchaguzi.