Stori Kubwa

Taarifa inayomuhusu mama aliyewaua watoto wake wawili Tabora iko hapa

on

twoJeshi la Polisi linawashikilia watu wawili wakazi wa Manispaa ya Tabora kwa tuhuma za kuwanyonga watoto wawili hadi kufa, kisha kuwafukia ndani ya nyumba waliyokuwa wanaishi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Juma Bwire, amethibitisha jana kutokea kwa mauaji hayo ya kikatili na kuwataja watuhumiwa kuwa ni mama mzazi wa watoto hao, Zuhura Masoud (25) na baba yake Shaban Ramadhan (75) wakazi wa Kata ya Chemchem mjini Tabora.

Baada ya mama huyo kutekeleza unyama huo, aliwafunga kwa kuwavingirisha kwenye mifuko ya sandarusi watoto hao Mwamvua Mrisho (4) na mwingine aliyetambuliwa kwa jina moja la Sudi kisha kuwafukia chini, mmoja sebuleni na mwingine chumbani kwake”:-Bwire.

suzan

Kamanda wa Polisi Tabora Suzan Kaganda

Tulipata taarifa tukazifanyia kazi kwa weledi wetu na kubaini ukweli wa mauaji hayo. Huyu mwanamke na baba yake mzazi mzee Ramadhani tunawashikilia kwa mahojiano zaidi na tunazo taarifa kwamba walikuwa wakigombea nyumba, inawezekana ugomvi huo labda ndiyo chanzo halisi cha mama kuamua kuchukua uamuzi mgumu kama huo“:- Bwire.

Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments