Top Stories

Watoto wa shule ya msingi wafunga ndoa, mahari Elfu 50 “Wazazi na Washenga tumewanasa”

on

Katika hali isiyokuwa ya kawaida wakazi wa mtaa wa Afya katika Mji mdogo wa Katoro Mkoani geita wamejikuta wakipigwa na butwaa baada ya Mtoto wa kiume wa darasa la nne na wa kike wa darasa la pili kufunga ndoa,  imefanyika sherehe kabisa, Mtoto wa kike akiwa na shela, imekatwa keki na wamevalishana pete, huku mahari ikiwa ni Tsh Elfu 50 tu ambayo Baba wa Mzazi wa kiume anasema ameitoa kwa niaba ya Mwanae.

Majirani wa Mtaa huo wanasema walipopata taarifa hiyo walishikwa na butwaa, huku wengine wakitafuta namba za Polisi ili watoe taaarifa, jirani mmoja anasema hiyo ni kama vile kuwafundisha ngono Watoto hao, tena isitoshe mambo haya yanafanyika wakati huu ambapo Dunia inapambana na Janga la corona.

Mwenyekiti wa Mtaa huo Jonathan Kazungu amesema baada ya kupata taarifa hiyo amewakamata Baba wa Mtoto wa kiume na Bibi harusi na washenga, huku wengine akiwemo Mzazi wa Mtoto wa kiume wakikimbia na kutokomea kusikojulikana.

DAWA YA CORONA YAPELEKWA NIMR KUTHIBITISHWA “INAPONYA TUTAKUWA NA DAWA KAMA MADAGASCAR”

Tupia Comments