Timu za ambulence zimeondoka katika hospitali ya Emirati kusini mwa Gaza- kuwapeleka watoto 28 wanaozaliwa kabla ya wakati kwenye kivuko cha Rafah,idara usalama ya Palestina ilisema.
Watoto hao wachanga watatibiwa katika hospitali za Misri mara moja kwenye mpaka.
Tuliripoti mapema (tazama chapisho letu saa 6.32 asubuhi), jinsi Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) lilivyosema watoto hao walitishiwa na uwezekano wa kuambukizwa magonjwa makubwa, huku 11 wakiwa katika hali mbaya.
Maafisa wa afya awali walisema jumla ya watoto 31 waliozaliwa kabla ya wakati walikuwa wamehamishwa salama katika hospitali ya Emirati, haijulikani ni nini kimewapata watoto watatu kati ya hao.
Wakati huo huo, wagonjwa wengine waliojeruhiwa vibaya bado wamekwama katika hospitali ya al Shifa, siku chache baada ya vikosi vya Israel kuingia katika boma hilo.
Kuhama kwa watoto hao ni juhudi za pamoja kati ya shirika la misaada, WHO na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu.