Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linawashikiria watu 3 wa Familia moja watoto wa Mama mmoja kwa tuhuma za kumuuwa mama yao Mzazi aitwaye Bi.Belembe Tobija (70) Mkaazi kijiji na kata ya Nyaruyeye Tarafa ya Busanda Mkoani Geita kwa kumkata kata na vitu vyenye ncha kali Mpaka kupoteza maisha.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Geita Henry Mwaibambe amesema chanzo cha tukio hilo ulirthi wa mashamba kama madai kutoka kwa mama yao mzazi huku mama yao akiwa anawakatalia kuwapa mashamba hayo na kusema amekwisha kuwalea ni jukumu lao kutoka nyumbani na kwenda kujitafutia.