Top Stories

Watoto wamuua Mama yao na kumkata viungo vya mwili (+video)

on

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera linawashikilia Watuhumiwa watatu Wakazi wa Wilaya ya Kyerwa kwa tuhuma ya kumuua Bibi wa miaka 99 Frazia Rukera wakimtuhumu kuwa ni Mchawi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Tuntufye Mwakagamba amesema kuwa Watuhumiwa hao watatu ni Watoto wa kuzaliwa wa Bibi huyo ambae sasa ni Marehemu na kuongeza kuwa alikatwa kichwa, mikono na mguu na kuondoka na viungo hivyo.

“Kilichofanya tuwashikilie Watoto wake ni kwasababu walimtenga Mama yao wakimtuhumu kuwa anawaroga Wanafamilia” RPC Mwakagamba

Soma na hizi

Tupia Comments