Top Stories

Watoto watatu wauwawa na Simba wakichunga “Walikuwa wanatafuta Mifugo” (Video+)

on

Watoto watatu ambao ni wanafunzi wa Shule ya msingi Ngoile iliyopo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha wamefariki Dunia kwa kushambuliwa na Simba wakati walipokwenda kutafuta mifugo iliyotorokea porini baada ya kutoka shuleni.

Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha Justine Masejo amesema tukio hilo limetokea August 3 mwaka huu huku akibanisha kuwa mtoto mmoja amejeruhiwa katika tukio hilo na amelazwa katika Zahanati ya kata ya Olbalbal iliyopo wilayani Ngorongoro.

Kamanda Masejo amewataka Wazazi na walezi kutowapa majukumu ya kuchunga Mifugo karibu na maeneo ya hifadhi ili kuepusha kushambuliwa na wanyama wakali.

Ayo TV imekusogezea hapa video hii ufahamu kile kilichojiri katika tukio hilo lililopoteza Uhai Watoto wa tatu

 

DIAMOND AUMIZWA NA MANARA KUONDOKA SIMBA AFUNGUKA YA MOYONI “NIMEUMIA”

 

 

 

Soma na hizi

Tupia Comments