Watoto wawili Gilson John Charles (13) mkazi wa mtaa wa Mpera na Ramadhani Sabayi(10) mkazi wa kata ya Malolo manispaa ya Tabora wameripotiwa kujinyonga katika matukio mawili tofauti huku mmoja akidaiwa kufokewa na mama yake mzazi
Katika tukio la kwanzaGilson John Charles (13) anadaiwa kujinyonga hadi kufa kwa kutumia kamba ya chandarua iliyokuwa kwenye mti nje ya nyumba yao usiku wa kuamkia leo Disemba 16,2024 huku chanzo cha kifo hicho kikitajwa ni kufokewa na mama yake mzazi baada ya kukaidi agizo la kupika chakula.
Katika tukio la pili Ramadhani Sabayi 10) mkazi wa kata ya Malolo pia nae amejinyonga kwa kutumia kamba iliyotengenezwa kwa mfuko wa simenti huku mama mdogo wa marehemu akidai kuwa si mara ya kwanza kujaribu kufanya kitendo hicho na alipokuwa akiulizwa alisema kuwa anakuwa hajielewi Pindi anapofanya kitendo hicho.
Matukio hayo yamethibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Richard Abwao ambapo amesema marehemu alichukua uamuzi huo daada ya kukaidi agizo hilokutoka kwa mama yake mzazi.
“Leo katika mtaa wa Mpera,Kuna tukio limetokea kwa kijana aliyekuwa amemaliza elimu ya darasa la saba katika shule ya msingi Ipuli amekutwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya chandarua ambayo aliitundika katika mti nje ya nyumba yao sababu ya tukio hili ni kugombezwa na mama yake kutokana na kushindwa kuwapikia chakula ndugu zake pamoja na kufanya usafi wa nyumba,alitoweka nyumbani tangu asubuh ya Jana na leo asubuh amegundulika amejinyonga nje ya nyumba yao. ” SACP Richard Abwao