Leo October 10 2016 shule ya sekondari Tegeta iliyopo jijini Dar es salaam wanafunzi wake wamegoma na kuandamana kuelekea kwa mkuu wa shule kwa madai kuwa walimu hawangii madarasani kufundisha aidha miiundombinu ya shule hiyo kutokuwa ya kuridhisha yakiwemo madarasa na vyoo.
Baadhi ya wanafunzi wakizungumza na Ayo TV wamesema walimu wamekuwa hawaingii madarasa kwa muda sasa na hata mazingira ya shule si ya kuridhisha.
millardayo.com na Ayo Tv pia ilimpata afisa elimu wa manispaa ya kinondoni, Rogers Yacob ambapo ameeleza kuhusu mgomo huo wa wanafunzi hao na kwa jinsi watakavyoshughulika na madai ya wanafunzi hao, Afisa elimu amesema shule hiyo imekuwa ikiendeshwa kwa ada za wazazi na wazazi wamekuwa halipi ada kwa wakati hali iliyopelekea walimu kutolipwa mishahara yao hivyo wamekuwa hawaingii madarasani.
Unaweza kuangalia video hii hapa chini
ULIKOSA HII YA KAMANDA WA POLISI DSM KUTAJA HATUA WALIZOCHUKUA KWA ‘BLACK AMERICANS WALIOMJERUHI ASKARI WA JWTZ