Watu wenye silaha wamewauwa takriban watu 16 wakati wa shambulizi kaskazini magharibi mwa Nigeria, serikali ilisema Jumapili.
Washambuliaji hao walivamia eneo la Serikali ya Mtaa ya Zangon Kataf katika jimbo la Kaduna na kufyatua risasi Jumamosi baada ya makabiliano na polisi katika kituo cha ukaguzi, Yabo Ephraim, msemaji wa serikali ya eneo hilo aliambia shirika la habari la Associated Press.
Washambuliaji hao walivamia eneo la Zangon Kataf katika jimbo la Kaduna na kufyatua risasi Jumamosi baada ya makabiliano na polisi katika kituo cha ukaguzi, Yabo Ephraim, msemaji wa serikali ya eneo hilo aliambia jarida moja la AP.
Maafisa waliweka marufuku ya kutoka nje katika eneo hilo baada ya shambulio hilo.
Mashambulizi kama hayo si haba nchini Nigeria, haswa katika maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo ambayo yameathirika sana.
Mzozo wa wafugaji umeibuka na kuwa vikundi mbalimbali vyenye silaha vinavyofanya vitendo vya unyanyasaji, kukaidi hatua za serikali na usalama kwa miaka kadhaa sasa.