Katika taarifa ya wizara ya afya iliyotolewa jana jioni, watu 26 wameripotiwa kuambukizwa virusi hivi tangu Septemba 27 wakati mlipuko wa kwanza kabisa wa Marburg ulipothibitishwa nchini humo.
Waziri wa Afya Sabin Nsanzimana amesema wanawafuatilia zaidi ya watu 300 ambao wanadaiwa kuwa waligusana na wagonjwa waliofariki na wale waliothibitishwa kuambukizwa.
Baadhi ya miongozi iliyotolewa ni pamoja na kusimamishwa kwa muda kuwatembelea wagonjwa hospitalini, kudumisha usafi binafsi na kuepuka kugusana na watu wanaoonyesha dalili za virusi vya Marburg, hata hovyo shughuli za biashara zitaendelea kama kawaida.
Aidha shughuli za mazishi na maombolezo ya nyumbani pia zimepigwa marufuku wafiwa wakitakiwa kuepuka msongamano inayoweza kuongeza hatari ya kueneza virusi hivyo, ambapo pia ufunuaji wa jeneza hautaruhisiwa katika nyumba, makanisa na misikiti.