Top Stories

Watu saba wamefariki wakipinga Bobi Wine kukamatwa

on

Watu saba wamefariki Dunia nchini Uganda kufuatia maandamano ya kupinga kukamatwa kwa Mgombea wa Urais Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine.

Inaelezwa kwamba zaidi ya waandamanaji 40 wamejeruhiwa katika makabiliano hayo na Polisi, ambapo shirika la Msalaba Mwekundu nchini Uganda limesema kuwa wafanyakazi wake waliwasaidia watu 11 waliokuwa na majeraha ya kupigwa risasi.

Wakati huohuo, Wagombea urais kutoka Vyama vya Upinzani nchini Uganda wamesema kuwa wanasitisha kampeni zao hadi pale mgombea mwenzao Robert Kyagulanyi atakapoachiwa huru.

Wagombea hao wamesema ni vigumu kwao kuendelea na kampeni huku mgombea mwingine akiwa anaendelea kunyanyaswa na polisi kwa madai yasiyo na msingi.

SERIKALI YAWEKA WAZI MASHARTI YA KUZINGATIA UNAPONUNUA VIGAE, UGUMU, SIZE

Soma na hizi

Tupia Comments