Michezo

Watu sita wafariki nje ya uwanja Cameroon

on

Watu sita wameripotiwa kufariki na wengine kadhaa kujeruhiwa katika msongamano uliotokea nje ya uwanja unaochezwa mechi za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Cameroon.

Picha za video zimeonesha mashabiki waking’ang’ana kuingia kwa nguvu katika uwanja Paul Biya uliopo katika Mji Mkuu Yaounde.

Uwanja huo una uwezo wa kuwapokea watu 60,000, lakini kwasababu ya masharti ya kuzuwia maambukizi ya Covid ulipaswa kupokea 80% pekee ya watu hao.

Maafisa wa mechi waliripotiwa wakisema kwamba watu wapatao 50,000 walikuwa wakijaribu kuingia ndani ya uwanja huo.
Msongamano katika lango la uwanja ulisababisha “vifo vya watu sita na wengine kadhaa wamejeruhiwa”, aliripoti mtangazaji wa kituo cha televisheni cha Taifa.

Soma na hizi

Tupia Comments