Top Stories

“Watu wametega jiwe kwenye njia ya treni” DC awapa agizo zito Polisi

on

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Kisa Gwakisa ameiagiza kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya kuchunguza watu waliohusika na dalili za kutaka kuhujumu miundombinu ya reli huku akiwataka wenyeviti wa vijiji kuunda vikundi vya ulinzi shirikishi kwaajili ya kukagua usalama wa miundombinu hiyo mara kwa mara.

Gwakisa ametoa kauli hiyo baada ya kutokea kwa watu wasiojulikana kutega jiwe kwenye njia ya reli hali ambayo ingeweza kuleta athari kwa treni ya abiria inayopita wilayani hapa.

“Tukio kujitokeza mara mbili hii haivumiliki, naagiza Polisi wachunguze wakina nani walihusika na ile hujuma, watu wametenga jiwe kwenye njia ya treni, tambueni treni imebeba Watanzania wenzetu, undeni vikundi vya vijana viwe vinakagua njia kila treni inapotaka kupita” DC Korogwe

Soma na hizi

Tupia Comments