Top Stories

Watu wanaokufaa kwa njaa wengi kuliko wa Corona

on

Shirika la misaada la Oxfam limesema idadi ya Watu wanaokufa kutokana na njaa inaizidi ile idadi ya Watu wanaokufa kutokana na maambukizi ya virusi vya corona ambapo idadi ya wanaokufa njaa iliongezeka mara sita zaidi mwaka uliopita wa 2020.

Limesema idadi ya Watu wanaokabiliwa na njaa duniani kote imeongezeka kuanzia mwaka uliopita kutoka Watu wapatao milioni 20 hadi Watu milioni 155 na kwamba Watu 11 wanakufa kutokana na njaa kila dakika moja kwenye saa 24 na hivyo kuvuka idadi ya watu wanaokufa kwa Covid-19.

Shirika la Oxfam limeongeza kuwa wakati njaa ikiendelea kuua Watu kila dakika duniani, Nchi mbalimbali zimeongeza pesa kujihami kijeshi ambapo bajeti za Majeshi mbalimbali duniani ziliongezeka na kufikia dola bilioni 51 mwaka 2020.

Oxfam imezitaja Afghanistan, Ethiopia, Sudan Kusini, Syria na Yemen kuwa Nchi ambazo ndizo zilizopo kwenye hali mbaya na Raia wake wanakabiliwa na njaa kutokana na mizozo au vita ambazo zinaendelea ndani ya mataifa hayo.

HUZUNI MKE NA MTOTO WA TB JOSHUA WAMWAGA MACHOZI WAKIAGA MWILI

Soma na hizi

Tupia Comments