Watu wasiojulikana wamevunja vioo vya madirisha 12 katika shule ya Sekondari Kibedya Wilaya ya Gairo Mkoa Morogoro Madarasa ambayo yamejengwa kwa fedha za UVIKO 19.
Diwani wa kata ya Kibedya Benedicto Masatu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema katika Shule hiyo yamejengwa Madarasa 6 Kutoka mfuko wa COVID 19 hivyo watu wasiojulikana wamevunja vioo vya Madirisha 12 ambayo thamani yake bado haijafahamika.