Millard AyoMillard Ayo
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
  • Contact
Search
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Reading: Watu watatu wahukumiwa kifungo cha Maisha, Ajali ya Ndege ya MH17
Share
Notification Show More
Latest News
Picha: Rais wa Yanga na GSM Foundation wawafariji Wananchi wa Katesh wilayani Hanang ‘Waathirika wa Mafuriko’
December 5, 2023
Wapalestina 50 walimepotiwa kuuawa siku ya leo Jumanne
December 5, 2023
Nilikosolewa vikali nchini kwangu Argentina kwa kushindwa kunyakua taji-Messi
December 5, 2023
Ali Al Bulayhi huenda akafungiwa mechi moja kwa maneno machafu
December 5, 2023
Marekani itakataa kutoa viza kwa maafisa wa Uganda wanaotekeleza sheria dhidi ya LGBT+
December 5, 2023
Aa
Millard AyoMillard Ayo
Aa
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Search
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Follow US
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Millard Ayo > Blog > Top Stories > Watu watatu wahukumiwa kifungo cha Maisha, Ajali ya Ndege ya MH17
Top Stories

Watu watatu wahukumiwa kifungo cha Maisha, Ajali ya Ndege ya MH17

November 18, 2022
Share
2 Min Read
SHARE

Mahakama ya Uholanzi siku ya Alhamisi (Novemba 17) imewahukumu watu watatu kifungo cha maisha na kumwachilia mwingine kwa kosa la kudungua ndege MH17 ya shirika la ndege la Malaysia Airlines nchini Ukraine mwaka 2014, huku kukiwa na mvutano unaoongezeka kuhusu uvamizi wa Urusi.

Warusi Igor Girkin na Sergei Dubinsky na raia mmoja wa Ukraine Leonid Kharchenko ‘wamepatikana na hatia’ ya mauaji na kuhusika katika kuangusha ndege, Mrusi Oleg Poulatov ameachiliwa huru, jaji kiongozi Hendrik Steenhuis amesema. Watatu wa kwanza walipatikana na hatia bila kuwepo mahakamani, kwani wote wanne walikataa kuhudhuria kesi hiyo, iliyochukua miaka miwili na nusu.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kwa upande wake amekaribisha “uamuzi huu muhimu”. “Adhabu kwa ukatili wote wa Urusi – jana na leo – haitaepukika,” ameongeza.

Ndugu wengi wa wahanga kutoka kote ulimwenguni walisafiri kwenda kusikiliza hukumu kwa kesi hii iliyotarajiwa sana katika mahakama yenye usalama karibu na uwanja wa ndege wa Amsterdam-Schiphol, ambapo Boeing 777 iliruka Julai 17 2014. Upande wa utetezi au wa mashitaka unaweza kukata rufaa.

Abiria na wafanyakazi wote 298 walipoteza maisha wakati ndege hiyo kutoka Amsterdam kwenda Kuala Lumpur ilipodunguliwa mashariki mwa Ukraine, eneo lililokuwa likishikiliwa na watu wanaounga mkono Urusi, na kile waendesha mashtaka wanasema ni kombora lililotolewa na Moscow. Majaji waliamua kwamba Igor Girkinen, Sergei Dubinsky na Leonid Kharchenko wote waliwajibika kwa kusafirisha kombora la BUK kutoka kambi ya kijeshi nchini Urusi na kulipeleka kwenye eneo la tukio, ingawa hawakuhusika peke yao. Hakukuwa na ushahidi wa kutosha kuonyesha kwamba Oleg Pulatov, mshukiwa pekee aliwakilishwa na mwanasheria wake wakati wa kesi hiyo, alihusika, wamesema.

Source RFi

You Might Also Like

Picha: Rais wa Yanga na GSM Foundation wawafariji Wananchi wa Katesh wilayani Hanang ‘Waathirika wa Mafuriko’

Wapalestina 50 walimepotiwa kuuawa siku ya leo Jumanne

Marekani itakataa kutoa viza kwa maafisa wa Uganda wanaotekeleza sheria dhidi ya LGBT+

Vita dhidi ya watoto ‘kila kukicha’ kusini mwa Gaza-UNICEF

Zaidi ya Wapalestina 15,900 waliuawa – waziri wa afya wa Palestina

Edwin TZA November 18, 2022
Share this Article
Facebook TwitterEmail Print
Share
Previous Article Mkali Jux katuletea hii single yake mpya akiwa na Khanyisa & Yumbs ‘Wena’
Next Article NSSF yatangaza fursa za uwekezaji
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

You must be logged in to post a comment.

- Advertisement -

Latest News

Picha: Rais wa Yanga na GSM Foundation wawafariji Wananchi wa Katesh wilayani Hanang ‘Waathirika wa Mafuriko’
Top Stories December 5, 2023
Wapalestina 50 walimepotiwa kuuawa siku ya leo Jumanne
Top Stories December 5, 2023
Nilikosolewa vikali nchini kwangu Argentina kwa kushindwa kunyakua taji-Messi
Sports December 5, 2023
Ali Al Bulayhi huenda akafungiwa mechi moja kwa maneno machafu
Sports December 5, 2023

You Might also Like

Top Stories

Wapalestina 50 walimepotiwa kuuawa siku ya leo Jumanne

December 5, 2023
Sports

Nilikosolewa vikali nchini kwangu Argentina kwa kushindwa kunyakua taji-Messi

December 5, 2023
Top Stories

Marekani itakataa kutoa viza kwa maafisa wa Uganda wanaotekeleza sheria dhidi ya LGBT+

December 5, 2023
Top Stories

Vita dhidi ya watoto ‘kila kukicha’ kusini mwa Gaza-UNICEF

December 5, 2023
Show More
//

To be recognized as Africa’s leading and most trusted online media network providing quality content across all our media platforms by 2025

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

Millard AyoMillard Ayo
Follow US

© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.

Removed from reading list

Undo

Lost your password?