Kundi la wanajihadi limeripotiwa kuwavamia wanajeshi na raia zaidi ya Elfu Moja nchini Burkina Faso na kuua baadhi yao, kwa mujibu wa taarifa ya gavana Ram Joseph Kafando, wa jimbo la Tawori.
Gavana Ram amesema shambulio hilo lilitokea Agosti 9 bila kutoa maelezo zaidi hasa kuhusiana na idadi ya watu waliofaraiki na ikiwa wanajeshi ni baadhi yao.
Burkina Faso na mataifa jirani ya Mali na Niger yanaendelea kupambana na wimbi la wanajihadi eneo nzima la sahel, tangu kuchipuka kwa wanajihadi hao miaka 12 iliopita.
Pametokea mapinduzi mawili ya serikali nchini Mali, mawili nchini Burkina Faso na moja nchini Niger, viongozi walioendesha mapinduzi hayo wakituhumu serikali za awali kwa kukosa kubaliana na tatizo la usalama kutoka kwa wanajihadi.
Mataifa ya Mali, Niger na Burkina Faso yametangaza kukatisha uhusiano wao na mkoloni wao wa zamani nchi ya Ufaransa.