Zaidi ya watu 600 wenye Ulemavu mbalimbali wamekutana jijini Dar es Salaam katika Kongamano maalumu liliandaliwa kwa lengo la kuangalia na kujadili namna kuongeza fursa kwa wenye ulemavu hasa kupitia mikopo.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo Mbunge wa viti maalumu kupitia mkoa wa Dar es Salaam Stella Ikupa amesema Dkt. Rais amelizingatia kundi hilo na kuelekeza kuwa kila wakati inapotekea fursa basi wapewe kipaumbele zaidi ili waweze kufanya maamuzi sahii na kushiriki katika michakato ya maendeleo na kuimarisha uchumi wao.
” Serikali imekuwa sikivu na sana na sisi tumekuwa tukisaidia serikali hasa katika shughuli za kutetea watu wenye ulemavu na michakato ya kiserikali hasa kwenye majengo mengi sana miundombinu imebadilika, na Tumeiomba Serikali na Taasisi binafsi iangazie katika kuwawezesha makundi maalumu kwa lengo na wao waweze kushiriki katika michakato ya maendeleo na kuimarisha uchumi wa nchini” Amesema Mbunge Stella Ikupa.
Kwa upande wake Peter charlse Mshauri wa kiutalamu wa maswala ya watu wenye ulemavu Tanzania amesema mkutano huo umejuisha watu mwenye ulemavu 600 kutoka ndani ya jiji la Dar es salaam wakiwepo madiwani 60 wa viti maalimu na wakuteuliwa.
” Ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu bado ni mdogo ndomana wakamamuu kuwalika madiwani katika mkutano huo ili kuangalia changamoto ipi wapi na kuwajengea uwezo madiwani ili kuweza kuwashirikisha madiwani katika mipango yao ya maendeleo kupitia mabaraza yao ndani ya halmashauri “Amesema Mshauri Peter.
Hata hivyo naye Hamadi Abdallah komboza, mwenyekiti wa Taifa wa chama cha walemavu Tanzani amesema “changamoto kubwa kwa watu wenye ulemavu ni maswala mazima ya ajira huku akimuomba kamshina wa kazi na vyama venye ulemavu kufanya ukaguzi kwenye mashirika na taasisi ambazi zinapasqa kuajiri watu wenye ulemavu lakini bado hazija kidhi ili kuweza lueta msukumo zipelekwa mahakamani ikibidi ili watu wenye ulemavu waweza kuajiriwa”.