Watu watano zaidi wamekamatwa kwa tuhuma za kuhusika katika mashambulizi dhidi ya mashabiki wa soka wa Israel mjini Amsterdam, polisi wa Uholanzi wamesema.
Takriban washukiwa 63 walikuwa tayari wamekamatwa baada ya mashabiki wa Israel kushambuliwa katika mji mkuu wa Uholanzi siku ya Alhamisi kufuatia mechi kati ya Ajax na timu ya Israel Maccabi Tel Aviv.”
Waziri Mkuu wa Uholanzi Dick Schoof alisema Uholanzi itaelekeza nguvu zake zote katika kuwafikisha wahusika mbele ya sheria.
“Picha na ripoti za Amsterdam na yale ambayo tumeona wikendi hii ya mashambulizi dhidi ya Waisraeli na Wayahudi sio ya kushangaza na ya kulaumiwa,” alisema Jumatatu.
Schoof alisema polisi na waendesha mashtaka bado wanajumuisha maelezo ya kile kilichotokea.
Vijana waliokuwa kwenye pikipiki na kwa miguu walikwenda kuwatafuta mashabiki wa Israel siku ya Alhamisi, wakiwapiga mangumi na mateke kabla ya kukimbia, kulingana na meya wa Amsterdam.
Takriban watu watano walijeruhiwa katika mashambulizi hayo, ambayo yalilaaniwa kuwa ya chuki dhidi ya Wayahudi na viongozi wa Uholanzi na viongozi wa kigeni akiwemo Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.