Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesa amesema wameendelea kukamata magari zaidi yenye vyuma chakavu kwa tuhuma za wizi katika operasheni dhidi ya wahujumu miundombinu ya Serikali kama reli ya kisasa, miradi ya maji na barabara.
“Watu wasio waaminifu wakatili na wanyanyasa sasa wameingia kwenye miundombinu wakiiba vyuma chakavu, wanatoa kwenye SGR na reli, tumekamata watuhumiwa 26 wakisafirisha vyuma chakavu” RPC Pwani