fB insta twitter

‘Maofisa utumishi 1,500 hatarini kutumbuliwa’

on

Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter>>>@millardayo na Zote nakusogezea hapa chini.

Moja ya habari iliyoripotiwa ni hii kutoka gazeti la Habari Leo yenye kichwa cha habari ‘Maofisa utumishi 1,500 hatarini kutumbuliwa’.

Gazeti hilo limeripoti kuwa Serikali imeagiza wote waliotengeneza watumishi hewa wafunguliwe mashitaka mahakamani huku ikionya kuwa iko tayari kusimamisha kazi maofisa utumishi wote nchi nzima wanaofikia 1,500 katika sakata hilo.

Waziri wa nchi, ofisi ya Rais, utumishi na utawala bora, Angella Kairuki alisema hayo jana wakati alipokuwa akichangia mjadala wa hotuba ya mpango wa maendeleoo na bajeti ya Serikali kwa mwaka 2016/2017 bungeni mjini Dodoma.

Waziri Kairuki amesema tayari Serikali imeshatoa agizo hilo la kuwashitaki maofisa wote waliotengeneza watumishi hewa na ikibidi iko tayari kuwasimamisha kazi maofisa utumishi 1,500 waliofundishwa kazi hiyo na Serikali.

Kwa mujibu wa Waziri Kairuki mpaka mwishoni mwa May Serikali ilikuwa imebaini uwepo wa watumishi hewa 12,246 waliokuwa wakitafuna bilioni 25.06 kila mwezi.

Unaweza kuzipitia hapa habari nyingine kubwa kwenye magazeti ya leo June 21 2016

ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI JUNE 21 2016 KUTOKA AYO TV? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments