Watumishi tisa wamesimamishwa kazi katika Kitengo cha upimaji wa COVID – 19 kwa Wasafiri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere (JNIA).
Agizo hilo limetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Prof. Abel Makubi alipofanya ziara uwanjani hapo kukagua utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa juzi alipofika hapo akiwa ameambatana na Katibu mwenzake wa Wizara ya Uchukuzi.
Prof. Makubi amesema hakufurahishwa na kitendo cha utovu wa nidhamu, kilichofanywa na Watumishi cha kutokufika kazini bila kutoa taarifa rasmi kwa uongozi.
“Jana Watumishi wanane hawakufika na leo mmoja bila kutoa sababu ya msingi, jumla wanakuwa tisa, imeonekana hapa hili zoezi la baadhi ya Watumishi kutokuja kazini limekuwepo, sasa hii imenisikitisha sana kwa baadhi ya Viongozi kushindwa kuchukua hatua zinazostahili na kulindana kwa kuficha uozo”———Makubi
TAZAMA UZURI WA LOUNGE MPYA AIRPORT, WAZIRI AZINDUA “ATCL TUNAONGEZA NDEGE”