Watumishi wawili wa Afya wa Zahanati ya Ishihimulwa Rose Shirima na James Getogo waliohusika kwenye video ya mabishano iliyosambaa wamesimamishwa kazi kwa muda ili kupisha uchunguzi.
Watumishi hao wamesimamishwa kazi na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Uyui, Tabora Dr. Kija Maige ambaye amesisitiza kuwa wawili hawa wanapisha uchunguzi kwa mujibu wa kanuni ya 37 ya kanuni za utumishi wa umma za mwaka 2003.
Uchunguzi huo utashirikisha Mabaraza yao ya kitaalamu ambayo ni Baraza la Wauguzi Tanzania na Baraza la Wataalamu wa Maabara Tanzania na hatua zaid zitafuata baada ya kukamilika kwa uchunguzi huo.