Waumini katika hekalu la Shri Banke Bihari, lililopo huko Vrindavan Nchini India, walikusanyika ili kunywa Maji yaliyokuwa yakidondoka kutoka kwenye Sanamu ya Tembo, wakiamini kuwa ni Maji matakatifu kutoka kwa miguu ya Bwana Krishna ambaye ni miongoni mwa miungu ya kihindu.
Waumini hao walijawa na imani kuwa maji hayo ni “Charan Amrit” (maji matakatifu kutoka miguu ya Bwana Krishna), lakini ilibainika kuwa ilikuwa ni unyevu kutoka kwenye mfumo wa baridi wa hekaluni (AC) maji.
Video za kushangaza zilizoonyesha Waumini kadhaa wakisubiri kwa mstari mbele ya Sanamu hiyo ambayo imevuta hisia nyingi na kuchochea mjadala kuhusu tofauti kati ya imani ya kidini na mantiki ya kawaida, watu wengi walishangazwa na hatua ya Waumini kuamini kuwa Maji hayo ni matakatifu huku wakiona ni muhimu kunywa ili kupata baraka, Hekalu lililazimika kutoa taarifa rasmi ikiwataka Waumini waache kunywa Maji hayo, kwani yalikuwa ni maji ya AC ya Hekaluni na si Maji ya kidini kama walivyodhani.
Taarifa hiyo iliwafanya Watu wengi kujiuliza kuhusu mpaka wa imani na mantiki, huku wakihoji jinsi imani za kidini zinavyoathiri uamuzi wa Watu katika maisha yao ya kila siku.