Top Stories

Wavamia Polisi kutoka tunguli za waganga ziachiwe Songwe (video+)

on

Baadhi ya Wananchi wa kata ya Galula Wilayani Songwe  wamezingira Kituo cha Polisi ili kulishinikiza jeshi la Polis kuyaachia mabegi yenye zana za kazi za Waganga wa kienyeji ‘tunguli’ walizokamata katika msako wa kutokomeza wapiga ramli chonganishi.

Kamanda wa Polisi Songwe Janeth Magomi amesema kuwa alipokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa kituo cha Polisi Galula kuwa Wananchi walizingira kituo hicho baada ya kukamata mabegi yenye tunguli ili kulishinikiza Jeshi la Polisi kuyaachia mabegi hayo na kumshinikiza Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji kurejesha fedha walizokuwa wamechangishana ili kuwaita Waganga hao.

Wananchi hao walivamia kituo wakiwa na mawe fimbo na mapanga na kuzua taharuki iliyopelekea Polisi kutumia nguvu kuwatawanya ambapo Watu watatu walijeruhiwa na na wengine 29 kukamatwa na watafikishwa Mahakamani.

 

 

Tupia Comments