Top Stories

Wawili wakamatwa na meno ya tembo Kilo 25

on

JeshiI la Polisi mkoa wa Kipolisi Rufiji, linawashikilia watuhumiwa wawili kwa kukutwa na nyara za serikali, zinazodaiwa ni meno ya tembo , uzito wa kilo 25.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Rufiji ACP Protas Mutayoba amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Jana huko maeneo ya Utunge-Kisemvule Wilayani Mkuranga.

Mutayoba alieleza kuwa, waliwakamata watuhumiwa hao wawili mmoja ni mwanaume mwenye umri wa miaka 40 na mwingine ni mwanamke mwenye umri wa miaka 21 wakiwa na nyara za serikali zidhaniwazo kuwa ni meno ya tembo vipande 16 vyenye uzito wa kilo 25 ambapo thamani yake haijajulikana.

Aidha Kamanda Mutayoba amesema watuhumiwa hao wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AFIKA MSIBANI KWA MKE WA AUGUSTINO LYATONGA MREMA, ATOA NENO KWA FAMILIA

Soma na hizi

Tupia Comments