Habari za Mastaa

Video 2 zikimuonyesha Lil Wayne akitaka kupigana baada ya kurushiwa chupa

on

Screen Shot 2014-05-07 at 2.29.28 AMUnaambiwa usiku wa pambano la Mayweather na Maidana Lil Wayne alijikuta akiwa pembeni ya timu ya Maidana wakati yeye yuko upande wa Mayweather ambapo walipofika katikati wakati anawapisha jamaa wa Maidana wapite akatokea mmoja akamrushia chupa.

Kikiwa ni kitendo cha dharau ya hali ya juu Wayne alipigwa na chupa hiyo kwenye uso na bega kitendo kilichomkasirisha sana mpaka kutaka kupigana huku akimsaka alierusha hiyo chupa.

Watu wa pande zote mbili waliingilia kati kabla ngumi hazijaanza kupigwa baada ya Lil Wayne kushikwa na hasira sana na kushindwa kuvumilia.

https://www.youtube.com/watch?v=4lmhZKzZcho

https://www.youtube.com/watch?v=L-33SDDsCF0

Unataka stori kama hizi zisikupite? jiunge na mimi twitter instagram facebook kwa jina hilohilo la @millardayo na nitakua nakutumia kila zinaponifikia iwe usiku au mchana.

Tupia Comments