WAZALISHAJI wadogo wa mafuta ya kupikia mkoani Mbeya ambao wamekidhi vigezo vya ubora, wametakiwa kujitokeza kusajili bure bidhaa zao na kupata nembo ya ubora ya Shirika la Viwango nchini, TBS, ili bidhaa zao ziweze kukubalika katika soko la ndani na nje ya nchi.
Maofisa kutoka Shirika la Viwango nchini TBS wapo jijini Mbeya kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi wa kawaida, wajasiriamali wadogo na wafanyabiasha na ndipo.
Ofisa Masoko wa Shirika hilo , Debora Haule amesema wamekusudia kuwafikia wajasiriamali maeneo wanapofanyia shughuli zao katika masoko, magulio kutoa elimu ya udhibiti ubora wa bidhaa wanazozalisha na kuziuza.
Amesema zaidi ya wajasirimali 10,000 wa Mkoa wa Mbeya watapatiwa elimu ya matumizi ya nembo zilizothibitishwa ubora wa bidhaa wanazozalisha na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) sambamba na gharama bure za usajili wa bidhaa zao.
Musa Luhombero, amesema lengo la elimu hiyo kusaidia bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali ambayo tayari zimethibitishwa kwa nembo ya ubora kuaminiwa na wateja.
Baadhi ya wajasiriamali waliopatiwa elimu akiwemo Stella Mdemu amesema walishindwa kusajili nembo ya bidhaa zao wakihofia gharama za usajili, hivyo taarifa ya kwamba huduma hiyo inatolewa bure imeleta matumaini na watasajili.