August 3 2016 Umoja wa vijana chama cha ACT-Wazalendo umekutana na waandishiwa habari Dar es salaam na kuzungumzia changamoto zilizopo katika sekta ya elimu nchini ikiwa ni pamoja kitendo kilichofanywa na serikali kwa kuwasimamisha masomo wanafunzi wa Chuo kikuu Dodoma (UDOM) wasiokuwa na sifa na baadae kuwarudisha baadhi yao.
Akizungumza kwa niaba ya wanachama hao Kitentya Luth ambaye ni mratibu wa vijana ACT-Wazalendo amesema…>>>‘Katika uamuzi huo wa kuwafukuza watoto wa kimaskini kutoka UDOM kukaibuliwa lugha za udhalilishaji kwa kuwaita Vilaza bila kuangalia athari za kisaikolojia‘
‘Sisi kwa nafasi yetu kama vijana tunalaani vikali udhalilishaji huo mbali ya kulaani tunaitaka Serikali ituambie na kutujibu masuala matatu yakiwemo‘ –Kitentya Luth
- Je, ni kweli tatizo lilikuwa Udahili ambao haukukidhi vigezo au ni ukosefu wa fedha baada ya wafadhili kujitoa kama tunavyosikia?
- Mliwezaje kuwapata wanafunzi zaidi ya 300 mkidai wamekidhi vigezo vya kurudi chuo na tunafahamu 7000 walikosa sifa kwa matokeo yao kuwekwa hadharani?
- Serikali imewapeleka wanafunzi katika vyuo vingine, je, waliopelekwa walienda kuendelea na elimu waliyoanza awali au walikuwa na mwanzo mwingine
ULIIKOSA HII YA ZITTO KABWE KUHOJIWA NA POLISI KWA DAKIKA 138