Top Stories

Waziri ajiuzulu baada ya kugundulika aliigizilia Chuo

on

Waziri wa Kazi, Familia na Vijana wa Australia, Christine Aschbacher amejiuzulu baada ya kugundulika kuwa baadhi ya kazi zake za chuo amenakili mawazo ya wengine (Plagiarism).

Aschbacher alifanya Tasnifu ya kupata Shahada ya Umahiri ambayo tasnifu yake ilikutwa na wizi wa mawazo ya kitaaluma kwa kushindwa kuwaandika wahusika kwa usahihi na hakuwa na ufahamu wa lugha ya kijerumani.

Wizi wa Kitaaluma umegundulinga na Stefan Weber ambayo ni bloga na aliwasilisha uchunguzi wake Chuo Kikuu cha Bratislava akionesha kuwa sehemu ya tasnifu yalikuwa mawazo ya wengine ambayo wenye mawazo yao hawakutajwa.

Inaonekana ni suala la kawaida kwa wanasiasa wa mataifa yanayozungumza kijerumani kuiba kazi za kitaaluma ili kupata shahada zao. Karl Theodor zu Guttenberg na Annett Achavan waliwahi kuachia madaraka kwa kashfa kama hizo.

RAIS MAGUFULI ALIVYOMPOKEA RAIS WA MALAWI AIRPORT CHATO

Soma na hizi

Tupia Comments