Serikali kupitia Wizara ya Kilimo amewataka wabia katika sekta hiyo kushirikiana na Wizara pindi wanapotoa Fedha ili zielekezwe kwenye maeneo yenye uhitaji kwaajili ya kumkwamua Mkulima badala ya kuelekezwa kwenye semina na walsha.
Kauli ya wizara imetolewa na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe wakati akizindua mpango mkakati wa miaka kumi utakaoonesha mwelekeo wa serikali katika mazao ya Bustani sambamba na mwongozo wa zao la Parachichi unaohusisha sekta binafsi.
Bashe amesema Sekta ya Kilimo inalenga kutatua changamoto za wakulima ikiwa ni pamoja na miundombinu ya umwagiliaji, upatikanaji wa mbegu bora, uhifadhi, Barabara na miundombinu ya masoko.
“Miundombinu ya umwagiliaji, upatikanaji wa mbegu bora, uhifadhi, Barabara na miundombinu ya masoko.haya ndiyo matatizo ya wakulima , wadau wa maendeleo wamekuwa wakitusaidia kwenye maendeleo kwenye sekta ya Kilimo na mara nyingi tunaona fedha nyingi ambazo wamekuwa wakizileta haziendi kwenye mambo ya kimsingi, huu siyo muda wa sisi viongozi kuitana kwenye mikutano kila siku, siyo warsha za kuita wataalamu lazima fedha hizi zikatatue matatizo ya msingi” Hussein Bashe
Waziri wa Kilimo