Waziri wa TAMISEMI, Innocent Bashungwa leo ametangaza matokeo ya uchaguzi wa Wanafunzi wa Kujiunga na kidato cha tano Vyuo vya Ualimu na Vyuo vya Elimu ya Ufundi May 2022.
“Muhula wa kwanza kwa Wanafunzi wa kidato cha tano utaanza tarehe 13 Juni, 2022, hivyo, Wanafunzi wote waliopangwa kujiunga na kidato cha tano kwa mwaka 2022 wanapaswa kuanza kuripoti katika Shule walizopangwa kuanzia tarehe 13 Juni, 2022, siku ya mwisho ya kuripoti itakuwa tarehe 30 Juni, 2022”-Waziri Bashungwa
“Endapo Mwanafunzi atachelewa kuripoti nafasi yake itachukuliwa na mwingine aliyekosa nafasi na kwa kuzingatia kuwa uchaguzi wa Wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano na Vyuo vya Elimu ya Ufundi umefanyika kwa kuzingatia ufaulu na nafasi zilizopo katika Shule, hakutakuwa na fursa ya kufanya mabadiliko yoyote ya Shule kutokana na ukosefu wa nafasi kwenye Shule husika”- Waziri Bashungwa
“Fomu za maelezo ya mahitaji ya kujiunga na kidato cha tano (Joining Instructions) kwa Shule zote za kidato cha tano zinapatikana kwenye tovuti ya OR-TAMISEMI kupitia kiunganishi cha www.tamisemi.go.tz na kwa wale waliopangwa kwenye Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi watapokea maelekezo ya namna ya kujiunga kutoka katika Vyuo walivyopangwa”- Waziri Bashungwa
“Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa inapatikana kwenye tovuti ya Ofisi ya Rais -TAMISEMI ya www. tamisemi. go. tz na Baraza la Taifa la Elimu ya Mafunzo ya Ufundi ya www. nacte. go. tz”- Waziri Bashungwa