Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Doto Biteko amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani, Innocent Bashungwa kumchukulia hatua za kisheria mtanzania anedaiwa kukutwa na shehena kubwa ya nyaya za Tanesco, miundombinu ya SGR mkoani Pwani kisemvule
ameyasema hayo leo katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi njia ya kusafirisha umeme msongo wa kilovoti 400 kutoka chalinze hadi Dodoma
“Mkuu wa mkoa huko hapa na Waziri wa Mambo ya ndani nataka kuona yule bwana mwenye godawn ambaye ameiba miundombinu hii hatu za kisheria zinachukuliwa kwake ili iwe fundisho mimi sitaki kuingilia mambo ya uchunguzi acha yafanyike lakini nataka nione haki inafanyika kwa watanzania wanaokosa Nishati kwa sababu ya tamaa ya watu wa chache” Naibu Waziri Mkuu Biteko