Selemani Jafo (Mb). Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira amesema mkoa wa Dar es Salaam unakabiliwa na uharibifu wa mazingira ikiwemo kuchimba Mchanga na Kokoto.
Waziri Jafo ameyasema hayo wakati wa ziara yake maeneo ya Mbweni jijini Dar es Salaam ambapo pia ametoa maagizo kuchukuliwa hatua za kisheria kwa gari ambalo lilikutwa likibeba mchanga katika maeneo hayo.
Hatua ya Waziri Jafo kufika maeneo ya Mbweni inatokana na video aliyoiona ya uharibifu wa maeneo hayo kupitia Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mbweni.