Waziri mpya wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa leo saa moja na nusu asubuhi amefanya ziara ya kushtukuza katika ofisi za kitengo cha Ardhi za Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa ajili ya kujionea hali ya utendaji kazi ikiwemo wa Watumishi kuwahi kazini.
Waziri Jerry amewahimiza Watumishi wa jiji la Dodoma na Tanzania kwa ujumla kuzingatia kufika ofisini kwa muda uliopangwa na inapofika saa moja na nusu asubuhi huduma zianze kutolewa na sio ndio Watumishi waanze kuingia ofisini wakati huo.