Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo (Mb) ametoa ufafanuzi wa taarifa ya mapendekezo ya ukarabati wa jengo la madini katika Maonesho ya Mwl. J.K Nyerere (Saba saba) na kuitwa jina la Hayati John Pombe Magufuli ambapo pia imependekezwa kujegwa sanamu ya Hayati Magufuli.
Prof. Mkumbo ameeleza kuwa “Benki ya NBC ndio wadhamini wakubwa wa maonesho ya 45 ya saba saba, moja ya makubaliano ya udhamini huo ni kufanya ukarabati wa mabanda mawili kwa gharama ya Millioni 420 fedha za Benki ya Biashara ya Taifa (NBC) sio za Serikali wala za Mkopo, lakini ni sehemu ya udhamini wao”
Aidha, mabanda yanayokarabatiwa kwa udhamini huo hutajwa majina ya Marais wastaafu, moja ya banda la madini limependekezwa kutajwa jina la Magufuli na tumeomba kibali kwenye Mamlaka ili kutaja jina hilo.”
Prof. Mkumbo aliendelea kueleza kuwa “Moja ya mapendekezo ya Benki ya NBC, wakikarabati banda waruhusiwe kujenga na sanamu ya Hayati Magufuli, ni mapendekezo yao ambayo yamewasilishwa Serikalini yanasubriwa kufanyiwa kazi na hayajapata majibu kwahiyo nisisitize hakuna uamuzi uliofanyika lakini muhimu zaidi fedha zinazozungumuziwa milioni 420 sio fedha za Serikali ni fedha za NBC kama sehemu ya ufadhili wao”.