Waziri wa Nishati, January Makamba leo amewasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati kwa Mwaka 2023/2024 ambapo moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba yake.
“Hali ya uzalishaji wa nishati ya umeme nchini kwa sasa haiendani na mahitaji ya shughuli za kiuchumi na kijamii yanayoongezeka kwa kasi…kuna upungufu mkubwa wa miundombinu ya usafirishaji na usambazaji wa umeme. Vilevile, baadhi ya miundombinu ni chakavu na mingine imezidiwa na matumizi ikilinganishwa na ilivyokusudiwa” – Waziri wa Nishati, January Makamba
‘Serikali kupitia REA itasambaza majiko banifu 70,000 katika maneo ya vijijini na vijiji-miji (peri urban) yaliyotengenezwa kwa teknolojia ambayo ina ubunifu wa kupunguza matumizi ya kuni na mkaa na kuwa na ufanisi mkubwa, hivyo kupunguza uharibifu wa mazingira na uzalishaji wa hewa ukaa’ – Waziri wa Nishati, January Makamba