Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni leo amewasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa Mwaka 2023/2024 ambapo moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba yake ni kwamba hadi kufikia mwezi May, 2023 Watanzania 66 waliukana uraia wa Tanzania na kupewa uraia wa Mataifa mengine.
“Watanzania hao wamepewa uraia wa Mataifa mengine ikiwemo Canada (6), China (1), Hispania (2), India (3), Marekani (11), Namibia (1), Newzealand (2), Oman (12), Ubelgiji (1), Uingereza (2), Ujerumani (23), Uganda (1) na Umoja wa Falme za Kiarabu (1)”
“Hivyo, kwa mujibu wa Sheria ya Uraia Sura ya 357 Rejeo la 2002, wote walioukana Uraia wa Tanzania wanapoteza haki ya kuendelea kuwa Watanzania, katika kipindi kama hicho mwaka 2021/22 Watanzania 40 waliukana Uraia wa Tanzania”