Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amelieleza Bunge, kuiacha tume iliyoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan ifanye kazi yake kushughulikia stahiki za watumishi walioachishwa kazi kwa madai ya kukosa cheti cha kidato cha nne.
Hatua hiyo inatokana na swali la mbunge wa Ushetu, Emanuel Peter Cherehani, aliyetaka kujua kauli ya serikali kuhusu watumishi walioondolewa kazini kwa madai ya kutokuwa na cheti cha kidato cha nne.
Waziri Mkuu, Majaliwa alifafanua kuwa Rais aliunda timu kutoka Wizara ya Utumishi na Utawala Bora, pamoja na Tamisemi, ili kuwatambua wote waliotumikia kwenye nchi hii na kutoa agizo kwamba walipwe asilimia 5 ya pensheni waliyokuwa wakiichangia.